Bayern Munich wanaitamani saini ya mlinzi wa Chelsea, Branislav Ivanovic, lakini hawawezi kumsajili mpaka januari mwakani.
Nahodha huyo wa Serbia mwenye miaka 31 bado ana mazungumzo na Chelsea kuhusu kusaini mkataba mpya na mkataba wa sasa unaisha mwaka 2016.
Bayern wanamhitaji Ivanovic, lakini hawatarajii kuona Chelsea wanamuuza, lakini bado wanajua kuwa nyota huyo atakuwa huru mpaka kufikia januari.
Wakati huo huo Paris Saint-Germain wanatarajia kuweka mezani ofa ya paundi milioni 7 kwa Chelsea ili kumsajili mlinda mlango mahiri Petr Cech majira ya kiangazi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment