KOCHA
msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ amesema timu yao imefanya
maandalizi ya kutosha kuikabili Ruvu Shootings ya Pwani katika mechi ya ligi
kuu soka Tanzania bara inayopigwa leo jioni uwanja wa Taifa.
Mkwasa
amekiri wazi kuwa Ruvu Shootings ni timu yenye wachezaji mahiri na nidhamu ya
mchezo, hivyo walikaa chini kujiandaa kwa umakini.
“Tunacheza
na Ruvu Shooting, timu ambayo ilitupa shida raundi ya kwanza na tulitoka nao
suluhu. Ni timu yenye wachezaji mahiri
na nidhamu ya mchezo, tumejiandaa vizuri kuweza kuwakabili na kuhitaji
ushindi” Amesema Mkwasa na kuongeza: “Tambwe (Amissi) ataongoza mashambulizi,
hatuwezi kusema bayana mbinu tulizompa, lakini ana majukumu maalumu aliyopewa
na tumemuelekeza nini cha kufanya dhidi ya mabeki wanaotumia nguvu wa Ruvu
Shootings (Michael George Osei)”
Yanga
wanaongoza ligi kuu wakiwa na pointi 49 baada ya kushuka dimbani mara 22, wakati
Ruvu Shooting wao wako nafasi ya 5 wakijikusanyia pointi 29 kufuatia kucheza mechi 23.
Mechi
zilizopita, Yanga walishinda magoli 3-2 dhidi ya Stand United uwanja wa Taifa
na wapinzani wao (Shooting) walishinda 2-1 dhidi ya Mgambo JKT, hivyo kila timu
inaingia kwa nguvu ikichagizwa na ushindi waliopata.
0 comments:
Post a Comment