Tuesday, April 28, 2015


Simba waligoma kuingia vyumbani

SIMBA walifungwa magoli 2-0 na Mbeya City katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa aprili 18 mwaka huu uwanja wa Sokone Mbeya.
Mechi hiyo ilikuwa na vimbwanga vingi vilivyohusishwa na imani za kishirikina.
Tukio kubwa lilikuwa kwa wachezaji wa Simba na benchi la ufundi kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Huu ulikuwa mwendelezo wa tabia hiyo kwani kwenye mechi waliyofungwa 2-0 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani Tanga na ile waliyoshinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga hawakuingia vyumbani.
Taarifa iliyotumwa na TFF mchana huu inaeleza kuwa kutokana na matukio hayo, shirikisho hilo limeamua kuipiga Simba faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuzingatia Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (changing room) katika mechi namba 159 dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 

Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video