Mechi iliyopita kiungo hatari wa timu hiyo , Emanuel okwi
alifanikiwa kuipatia timu hiyo magoli matatu katika ushindi wa goli nne.
Goli moja likifungwa na winga mzawa Singano.
Ukiitazama Simba iliyocheza na Mbeya City na Simba iliyocheza juzi dhidi ya Mgambo JKT ni timu mbili tofauti.
Okwi alitengeneza kombinesheni nzuri na viungo wenzake hali
iliyoifanya timu hiyo ambayo bado ina ndoto ya kushika nafasi ya pili
kuwa nzuri. Mechi na Mbeya City Okwi aliikosa mechi hiyo baada ya kuwa
na kadi tatu za njano.
Lakini Ndanda FC wanaoshikilia nafasi ya 8 wakiwa na
pointi 28 bado wanahitaji sana pointi tatu kujihakikishia kutokushuka
daraja.
Ukitazama timu zilizoko chini yake , wanapishana kwa pointi chache sana kwa wastani wa game moja.
Ndanda watakaza sana leo dhidi ya Simba . Pia wanajua mechi ya mwisho ni mtihani kwao.
Ndanda tarehe 9 May , watamalizana na Yanga ambao wanaonesha nia ya kuubeba ubingwa huo kwa heshima kubwa.
Yaani hata kama Azam atapoteza leo kwa Stand na
kuihakikishia ubingwa Yanga , bado safu yake ya ushambuliaji inahitaji
kuandika historia kwa wingi wa magoli.
0 comments:
Post a Comment