KLABU ya Simba imeshuka kiuchumi kutokana na mashabiki wake
kutohudhuria viwanjani pindi timu yao inaposhuka dimbani katika mechi za ligi
kuu soka Tanzania bara iwe jijini Dar e salaam au mikoani.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Zacharia Hans
Poppe amethibitisha klabu ya Simba kushuka kiuchumi na kusema mzigo umewalemea
sana kwa wakati huu.
“Tumefanya ulinganifu wa msimu uliopita na msimu huu,
tunaona idadi ya watu wanaokuja kuangalia mechi imepungua sana, hata kama timu
haifanyi vizuri kupata milioni sita, tano katika mechi ndogo ilikuwa kawaida,
lakini haijawahi kutokea tunacheza Taifa tunapata laki mbili, tumecheza na
Ndanda tumepata kiasi hicho”. Amesema Hans Poppe.
Alipoulizwa kwanini mashabiki wa Simba hawafiki kwa wingi
uwanjani?
Hans Poppe ameeleza kuwa: “Unajua watu wengi hawahudhurii
mechi kwasababu hawana sababu ya kukata tiketi, mbona msimu uliopita tulifanya
vibaya lakini walikuwa wanafika uwanjani?, mashabiki wengi waliokuwa wanakuja
kuangalia mechi, panga pangua huwa hawakosi mechi,sasa hivi wengi wao wanasema
tutakuja kufanya nini uwanjani wakati kuna ving’amuzi vya Azam TV mahali kote”
Azam TV ndio televisheni pekee yenye haki za kurusha
matangazo ya mechi za ligi kuu soka Tanzania bara, lakini Hans Poppe anaitaja
kuwa sehemu ya kushusha mapato ya Simba na klabu nyingine za ligi kuu.
Je, kweli Azam TV ndio sababu ya mashabiki wa Simba kutofika
uwanjani? Tupia maoni yako hapa….
0 comments:
Post a Comment