SIMON
msuva, winga hatari, mwenye kasi kubwa amesema leo anaandika historia ya
kuchukua ubingwa kwa kufunga magoli mengi leo wakichuana na Polisi Morogoro
uwanja wa Taifa.
Nyota
huyo aliyefunga goli linaloelekeana na la Robin Van Persie kwenye michuano ya
kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil amesema amejiandaa vizuri kuongeza
idadi ya magoli.
“Namshukuru
Mungu nafanya vizuri msimu huu, naongoza kwa magoli 16, sijaridhika, napambana
kufunga mengi zaidi”. Amesema Msuva na kusisitiza: “Leo hatufanyi makosa,
tunamaliza biashara mapema, naamini mashabiki wa Yanga watafurahia kazi nzuri
tutakayofanya”.
0 comments:
Post a Comment