KOCHA wa Polisi Morogoro John Tamba ametupiwa lawama na
nahodha wa timu hiyo Nicolaus Kabipe kwa kuwaacha benchi baadhi ya wachezaji
ambao wangeweza kushindana na Yanga jana uwanja wa Taifa akiwemo yeye.
“Makocha wetu bwana sijui wanawaza nini, hivi kwanini
alituacha wengine? Tumewapa Yanga cha kusema, Si umeona nilivyoingia mimi, Nahoda
Bakari tulibadilisha timu na kufunga goli moja? Ningekuwepo toka mwanzo
ningewasumbua sana Yanga”. Ametamba Kabipe aliyekuwa chaguo la kwanza mbele ya
kocha aliyetimuliwa Adolf Rishard.
Kabipe amesikitishwa sana na kipigo cha magoli 4-1
walichopata jana kutoka kwa Yanga na amesema sasa matumaini ya kubaki ligi kuu dhahiri
yamekwenda na maji.
“Tuna kazi ngumu ya kufanya dhidi ya Mbeya City katika mechi
yetu ya mwisho, tunajua wenzetu (Mbeya City) wamepumua kwa matokeo ya mechi
mbili zilizopita, tutaenda kupambana na kuona nini kitatokea”. Ameongeza
Kabipe.
Wakati huo huo Mtandao huu ulimuuliza John Tamba kwanini
aliwaacha benchi baadhi ya wachezaji akiwemo Kabipe?
Tamba alieleza kuwa kila mchezo una mpango wake, anapanga
mchezaji kutokana na aina ya timu anayokutana nayo.
“Kubadilisha kikosi ni jambo la kawaida, sioni kitu cha
ajabu. Kila mchezo una mpango wake, nilipanga kikosi kulingana na aina ya
wapinzani wangu, kufungwa sio sababu ya kusema nilikosea kupanga timu”
Amejitetea Tamba.
0 comments:
Post a Comment