Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Okwi ndiye kinara wa mabao Simba kwa sasa licha ya kukosa mechi kadhaa ikiwemo waliopigwa 2-0 dhidi ya City Jumamosi.'
HAT-trick yake ya ndani ya dakika 50 aliyoipiga jana dhidi ya Mgambo Shooting Stars, imemfanya kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, kuwakamata Amissi Tambwe wa Yanga, Rashid Mandawa wa Kagera Sugar na Didier Kavumbagu wa Azam FC katika safu ya wafumania nyavu hatari zaidi msimu huu.
Okwi, mchezaji wa zamani wa SC Villa ya kwao Uganda, Etoile Sportive du Sahel (ESS) ya Ligi Kuu ya Tunisia na Yanga, alifungta hat-trick hiyo katika ushindi wa 4-0 wa Simba dhidi ya Mgambo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini hapa.
Mabao hayo matatu yamemfanya Okwi afikishe mabao 10, hivyon kuwakamata washambuliaji hao watatu wanaokamata nafasi ya pili katika safu ya watupiaji magoli hatari msimu huu wakiongozwa na kiinara Simon Msuva wa Yanga SC wenye mabao 14.
Hat-trick ya Okwi imeifanya Simba kuwa na hat-trick mbili msimu huu baada ya Ajibu kuwafungulia njia Februari 28.
Jambo jingine la kufurahisha ni kwamba, hat-trick zote zimefugwa kwenye Uwanja wa Taifa jjini hapa.

0 comments:
Post a Comment