Thursday, April 23, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Okwi amekuwa mchezaji wa tatu kuondoka na mpira msimu huu baada ya Ibrahim Ajibu wa Simba na Amissi Tambwe wa Yanga kufanya hivyo.'
MSEMAJI wa Simba, Haji Manara, amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, aliahidi kupiga hat-trick katika mechi yao ya jana dhidi ya Mgambo Shooting Stars iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini hapa.
Manara amedai kuwa Okwi aliuahidi uongozi kwamba alikuwa anakwenda kufunga mabao matatu jana.
"Okwi ni mchezaji wa aina yake, alituahidi viongozi kwamba atapiga hat-trick katika mechi ya jana na kweli akafanya hivyo. Hakuna mchezaji wa kimataifa Tanzania ambaye anaweza kumfikia Okwi kwa sasa," ametamba Manara katika mahojiano na mtandao huu jijini hapa muda mfupi uliopita.
Okwi hakuzungumzia ahadi hiyo katika mahojiano na mtandao huu mara tu baada ya kumalizika kwa mechi hiyo jana.
Lakini, anachokisahau Manara ni kwamba, wachezaji wengine wa kigeni nchini wamefanyab kazin kubwa katika klabu zao msimu huu na hata msimu uliopita kuzidi hata Okwi anayemsifia.
KIPRE TCHTECHE -AZAM FC
Mshambuliaji Kipre Tcjetche wa Azam FC alifanya kazi kubwa msimu uliopita na kuipa timu yake taji la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) tangu ipande ligi kuu 2007. Raia huyo wa Ivory Coast pia aliibuka mchezaji bora msimu uliopita.
Bila kusahau pacha huyo wa Kipre Bolou wa Azam FC pia, aliibuka mfungaji bora wa VPL msimu wa 2012/13 akifunga mabao 17. Okwi hajawahu kuibuka mfungaji bora wa ligi hii hata msimu mmoja.
Hata kwa sasa, Tchetche bado ana mchango mkubwa katika kikosi cha Azam FC na anapokosekana uwanjani timu hiyo imekuwa ikipata matokeo mabovu. Katika mechi ambazo hakucheza msimu huu, Azam FC ilifunga 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Stars, 1-0 dhidi ya Ndanda FC na suluhu dhidi ya Mgambo Shooting Stars.
AMISSI TAMBWE - YANGA
Wakati Manara anamuona Okwi ni zaidi ya wachezaji wote wageni wa VPL, takwimu zinathibitisha kwamba mtazamo huo ni butu. Mashambuliaji wa Yanga, Mrundi Anmissi Tambwe aliibuka mfungaji bora wa VPL msimu uliopita akifunga mabao 19 katika mechi 23 kati ya 26 alizopangwa katika kikosi cha Simba, mabao ambayo hayajawahi kufungwa na Okwi katika msimu mmoja, tena katika mashindano yote.
Tambwe pia msimu huu tayari ameshafunga mabao 10 msimu huu wa VPL sawa na Okwi na ana mabao mengine mawili katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.
Mbali na kuibuka mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, Tambwe alikuwa mfungaii bora wa Kombe la Kagame 2013 akiwa na Vital'O ya kwao Burundi aliyoifungia mabao sita nchni Sudan na kuipan taji la mashindano hayo ya Ukanda wa CECEFA.
Kabla ya kujiunga na Simba mwaka juzi, Tambwe pia aliibukia mfungaji bora wa Ligi Kuu ya kwao Burundi. Mrundi mwenzake pia Didier Kavumbagu wa Azam FC mwenye mabao 10 msimu huu sawa na Okwi na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC, naye ana mchango mkubwa katika klabu yake a VPL kwa ujumla.
Kwa kifupi, kauli ya Manara haijazingatia tafiti na takwimu za soka zilizopo. Nafasi anayocheza Okwi ni tofuati na nafasi anayocheza Tambwe. Huwezi kuwalinganisha wawili hao na kusema mmoja ni zaidi ya mwenzake.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video