MWEZI mmoja umepita tangu gazeti la udaku la Hisania, Hola, kufichua mapenzi mapya ya mchezaji wa Manchester United, Javier Hernandez.
Nyota huyo wa miaka 26, raia wa Mexico alijiunga Santiago Bernabeu mwezi septemba mwaka 2014.
Hernandez 'Chicharito' alijiunga Real Madrid kwa mkopo wa muda mrefu huku kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja baada ya mkopo kumalizika.
Kama mshambuliaji huyo ataendelea kuitumikia Real Madrid mwaka ujao haijulikani, lakini gazeti la Hola limeeleza kuwa Chicharito ana nia ya kuendelea kubaki Real Madrid.
Lucia Villalon ambaye ni mtangazaji wa Real Madrid TV aliwahi kuhusishwa kuwa na mapenzi na Cristiano Ronaldo, lakini sasa anahusishwa kuwa na mahusiano na Chicharito.
Baada ya Chicharito kufunga goli la ushindi dhidi ya Atletico Madrid kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya jumatano ya wiki hii, alionesha ishara kwa msichana huyo aliyekaa katikati ya umati wa watu.
Kwa furaha kubwa, Lucia Villalon alirudisha ishara akiwa kwenye kiti chake katikati ya umati wa watu.
Tazama picha chini:
0 comments:
Post a Comment