SIMON Happygod Msuva amesema anajisikia furaha kuchukua
ubingwa huku goli lake la kichwa alilofunga kwa kichwa dhidi ya Ruvu Shooting
likijadiliwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kufananishwa na alilofunga
mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi, Robin van Persie kwenye fainali
za kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil.
Msuva (kulia) akiwa na Mrisho Ngassa
Msuva (kulia) akiwa na Mrisho Ngassa
“Watu wanasema nilifunga kama Robin Van Persie, wanajadili
sana kwenye mitandao, haya ni mafanikio kwangu, juhudi ndio siri ya mafanikio”
Amesema Msuva.
Winga huyo anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa amefumania
nyavu mara 17 msimu huu akifuatiwa na Amissi Tambwe mwenye magoli 14 ameongeza
kuwa ubingwa waliopata anafurahi kuchangia kwa kiasi kikubwa na ataendelea
kufanya vizuri.
“Huu ni mwanzo tu, kila siku najifunza na kupunguza makosa,
tuna kocha mzuri, tunaamini tutafanya vizuri zaidi siku zijazo tukianzia na
mechi ijayo dhidi ya Etoile du sahel”. Amesema Msuva.
0 comments:
Post a Comment