Baadhi ya mashabiki walimshutumu Manyika Jr kushuka kiwango
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
‘Manyika Jr ameingia mgogoro na Simba SC baada ya kuweka picha za mpenzi wake kisha kuwatusi wapenzi wac klabu hiyo kwa kusema: “Anayesema huyu ananishusha kiwango aje adake yeye…’
UJEURI mwiko Simba, nidhamu ndiyo kila kitu. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana benchi la ufundi la wekundu hao wa Msimbazi kuanika sababu za kumpanga kikosini kipa kinda kutoka kikosi B, Said Lubawa, badala ya kinda mwingine, Peter Manyika Jr.
Katika kikosi cha kwanza cha Simba kilichoibamiza Mgambo Shooting 4-0 Uwanja wa Taifa jijini hapa, kipa mkongwe Ivo Mapunda ndiye alitekuwa langoni badala ya Manyika Jr ambaye alifungwa katika kipigo cha 2-0 dhidi ya City jijini Mbeya Jumamosi.
Dennis Richard
Dennis Richard
Katika orodha ya wachezaji saba wa akiba alikuwa Lubawa akiwa ni kipa wa akiba huku Manyika Jr asionekane hata benchini kwa mara ya kwanza tangu msimu huu uanze Septemba 20, mwaka jana.
Akizungumzia suala hilo mara tu baada ya mechi hiyo kumalizika, kocha mkuu wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic, alisema Lubawa pia ana uwezo mkubwa na angeweza kuanza dhidi ya maafande hao wa Kabuku, Handeni jinini Tanga endapo Mapunda asingekuwa katika hali nzuri.
0 comments:
Post a Comment