Saturday, April 25, 2015

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amenukuliwa akisema kuwa haoni kama kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ni mpinzani wake.
Makocha hao wawili wamekuwa na tabia ya kurushiana vijembe mara kadhaa, lakini Mourinho amesema kuwa haoni haja ya kubishana na Wenger hasa wakati huu ambao wanatarajia kukutana katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza wikiendi hii.
"Kwangu, Wenger sio mpinzani wangu, Mourinho aliwaambia wanahabari. "Mimi sidhani kabisa. Najua yeye ni kocha wa klabu kubwa ambapo pia timu yangu ipo.
"Sasa kwa sababu hiyo basi, ndiyo maana unakuta kuna upinzani, Lakini sioni tofauti ya Wenger na kocha wa Atletico Diego Simeon wakati ule nipo Real Madrid."
Mourinho ana rekodi nzuri sana mbele ya Wenger, huku wakikutana mara 12 lakini hajawahi kufungwa hata mchezo mmoja, lakini akasisitiza kuwa haoni kama kuna haja ya kujivunia rekodi yake hiyo nzuri mbele ya wenger.
"Kwangu, mafanikio ni kushinda kesho," aliongeza.
"Suala hapa sio kuhusu michezo 12 ambayo tumewahi kukutana hapo kabla. Siangali hilo mimi. siagalii mambo ya idadi mimi. Na pia siangalii nilichokifanya dhidi ya kocha ama klabu yenyewe."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video