DAVID Mwamwaga, kocha wa zamani wa Simba, JKT Ruvu
na Tanzania Prisons kabla ya kumuachia jumba bovu kocha wa sasa Mbwana Makata
amesema milango ipo wazi kwa timu yoyote inayomhutaji.
“Mpango wa baadaye ni kwamba kama timu yoyote
itajitokeza kunihitaji basi nitafanya kazi, milango iko wazi kabisa, yaani ya
mbele na nyuma. Sijaitolea macho klabu yoyote, lakini liko wazi kwamba timu itakayonihitaji
nitafanya kazi”. Amesema Mwamwaja na kufafanua: “Unajua kufundisha soka ni
shughuli ya uzoefu, unaweza kufanya vibaya au vizuri, lakini haina maana huwezi,
bado ninaendelea kupambana”
0 comments:
Post a Comment