Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire akionekana mwenye mawazo baada ya timu yake kupokea kipigo kitakatifu cha mabao 5-0 kutoka kwa Yanga.
Masau Bwire haishiwi hadithi, jana ametoa kali ya mwaka pale alipowageuzia ubao Yanga na kuwapa hadithi nzuri ya ya mvuvi na samaki.
Alitamba kwamba timu yake haiwezi kufungwa na kufanywa njia ya Yanga kwenda kuchukua ubingwa. Lakini baada ya kipigo, akawataka Yanga wasishangae.
"Mambo yanakwenda yanabadilika, ni kama mvuvi ambaye amejaribu kutupa nyavu zake, akivuta anakuta hakuna samaki, anarudia tena hapati samaki.
"Si kila siku ni Ijumaa, mambo yanabadilika. Ni kawaida kabisa, sasa msione ajabu na sisi bado tuko imara kabisa," alisema Bwire na kufanya kauli yake hiyo kuwa gumzo kwelikweli.
Hata hivyo, picha inamuonyesha akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa wakati akishuhudia kipigo hicho kutoka kwa Yanga.
0 comments:
Post a Comment