UONGOZI wa Bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB)
umewatahadharisha mabingwa wa ligi kuu msimu huu 2014/2015, Dar Young Africans
kutojihusisha na upangaji wa matokeo katika mechi zao mbili zilizosalia.
Yanga watacheza na Azam fc uwanja wa Taifa aprili 6 mwaka
huu na kumalizia ligi uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara dhidi ya
wenyeji Ndanda fc mei 9 mwaka huu.
Mechi ijayo haina
faida wala athari yoyote kwa Yanga, lakini inaweza kuwaharibia zaidi Azam kama
watafugwa kwasababu itakuwa inatoa mwanya kwa Simba kuiwania nafasi ya pili.
Lakini kwa vile Yanga ni maadui wa kimpira wa Simba na
hawataki wapande ndege mwakani kwenye mashindano ya CAF, kuna maneno ya hapa na
pale kwamba Wanajangwani wanaona bora kufungwa na Azam ili kuwatengenezea
mazingira ya kuchukua nafasi ya pili lakini sio watani wao wa jadi Simba.
Machi 8 mwaka huu, Yanga ilifungwa goli 1-0 na Simba kwenye
mechi ya ligi kuu na kipigo hicho kimetia doa ubingwa wao, hawafurahii kuchukua
ubingwa huku wakiwa wamefungwa na Simba.
Mwenyekiti wa Bodi ya ligi kuu, Ahmed Yahya amewataka Yanga
kucheza mpira kwa kufuata kanuni na sheria za mchezo katika mechi zao zilizosalia.
“Yanga wajijue kuwa bado wana jukumu katika ligi hii, mechi
hazijamalizika, wacheze mpira, wanaweza kushangilia ubingwa halafu mwisho
wakaanza mambo ya maajabu, wakatuharibia ligi yetu
“. Amesema Yahya na kuongeza: “ Nina maana kwamba wao wameshakuwa mabingwa,
wanaweza kuona hawana majukumu tena katika ligi hii, wao waendelee kucheza
mpira uwanjani na kujiepusha na mipango ya nje ya uwanja” Amesema Yahya.
0 comments:
Post a Comment