Jumla ya timu 20 zinazoshiriki ligi ya England zinatarajiwa kushuka dimbani mwishoni mwa wiki hii.
Hata hivyo mechi ya Chelsea na Arsenal ,inaoonekana kuwa na
mvuto zaidi kwa wengi, kufuatia matokeo ya mechi hiyo kutoa picha mbili
tofauti, moja kuihakikishia Chelsea ubingwa iwapo itashinda mechi hiyo .
Na pia Arsenal ikishinda italeta
mazingira ya wazi kwa timu yoyote kati ya timu hizo mbili kutwaa
ubingwa.
Naye kocha Liverpool Brendan Rodgers ameibuka na kutamba
kuwa yeye ni kocha bora na hakuna kama yeye, huku akisema anamatumaini
ya kuendelea kukinoa kikosi.
Pamoja na majigambo hayo Rodgers ameweka rekodi mpya ndani
ya klabu hiyo kwa kuongoza misimu mitatu bila kuchukua taji lolote,
tofauti na watangulizi wake tangu mwaka 1950.
0 comments:
Post a Comment