Mbwana Makata (wa kwanza kulia) akiiongoza timu yake kwa moja ya mechi za ligi kuu.
KOCHA
mkuu wa Tanzania Prisons, Mbwana Makata bado hajakata tamaa ya kubaki ligi kuu
licha ya timu yake kuwa dhoofu katika msimamo mpaka sasa.
Prisons
ndio timu iliyofanya vibaya zaidi msimu huu ikiwa na pointi 22 mkiani baada ya
kucheza mechi 23, lakini kocha wake (Makata) amesema: “Tuna mechi tatu ambazo
zitaamua hatima yetu ya kubaki au kushuka daraja, niliichukua timu ikiwa mazingira
magumu, lakini mimi kama mwalimu ni kama daktari, unamchukua mgonjwa ambaye
yuko mahututi unajitahidi kuhakikisha unamponya. Ukiweza kuokoa maisha yake
unaonekana bingwa na ukishindwa unaumia”.
“Nitapambana
sana, wanaojua mpira wa miguu wanajua nilichukua timu katika wakati gani, timu
ilikuwa na pointi 11, kwahiyo atajua nilichokifanya, nitapambana kuhakikisha
tunabaki”.
0 comments:
Post a Comment