Jerry Muro
SIKU moja tu baada ya Yanga kutwaa ubingwa, msemaji wa Simba
, Hajji Sunday Manara amesema atatembea bila nguo kuelekea jangwani na kuwapigia
magoti kama watawafunga wapinzani wao wa kombe la shirikisho Etoile du Sahel.
Etoile na Yanga zitarudiana mwishoni mwa juma hili huko
Tunisia katika mechi ya hatua ya 16 bora ya kombe la shirikisho na mechi ya
kwanza jijini Dar es salaam timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Ili kusonga mbele moja kwa moja Yanga inahitaji ushindi au
sare ya kuanzia magoli 2-2.
Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
leo amejibu mapigo kwa Hajji Manara, mtoto wa zamani wa mchezaji wa Yanga,
Sunday Manarea ‘Computer’.
“Tunakwenda Tunisia kuhakikisha tunapata ushindi na kusonga
mbele japokuwa tunajua kuwa mwakani tutacheza ligi ya mabingwa kwasababu sisi
ni wa kimataifa”. Amesema Muro na kuongeza: “Lakini niweke kumbukumbu sawa kuwa
jana kuna kiongozi mmoja wa timu ya mchangani (Simba) alisema tukifungwa
atakuja klabuni kwetu bila nguo, mimi namwambia aanze maandalizi mapema, najua
anavaa kofia, kesho aanze kutoa kofia, keshokutwa aanze kutoa shati, yeye
anasema hivyo kwasababu anajua alizaliwa jangwani, ni mtoto wa jangwani, yeye
anatafuta namna ya kurudi jangwani, arudi jangwani aje ale mayai na mikate,
hapa ni kwao, huko kwingine anaganga njaa tu”.
Yanga jana waliifunga Polisi Morogoro na kufanikiwa kuchukua
ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi
kufikiwa na timu yoyote, huku ikisaliwa na mechi mbili dhidi ya Azam fc na
Ndanda fc.
0 comments:
Post a Comment