Abdi Banda (kushoto) alitunishiana msuli na Nadir Haroub 'Cannavaro' wa Yanga machi 8 mwaka huu Simba ikishinda 1-0
KIUNGO mkabaji wa Simba, Abdi Hassan Banda
anasumbuliwa na marelia na jana aliukosa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, Mnyama akishinda 4-0 dhidi ya Mgambo JKT
uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Magoli ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi
(Magoli matatu, Hat-trick) na moja lilifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Banda ameongea na MPENJA BLOG na kuweka wazi:
“Najisikia marelia siku ya pili sasa, nimeona ningelazimisha kucheza labda
ningepata matatizo ya kiafya au kutoonesha kiwango kizuri. Bora nikaa nje ya
uwanja tu. Tulipotoka Mbeya ndipo nilisikia kuumwa”.
Hata hivyo inaelezwa kuwa kocha mkuu Goran
Kopunovic alimwambia Banda atatumika kwenye mechi hiyo na baada ya kuelezwa na
mchezaji kuwa hajisikia vizuri kucheza, kocha akasikitika.
Banda amekuwa akicheza vizuri kwenye mfumo wa
4-3-3 ambayo kocha Goran Kopunovic anapenda kuutumia na wamekuwa wakicheza
vizuri sana na Jonas Mkude.
Anampanga Mkude kiungo cha nyuma, mbele yake
wanacheza Banda na Said Ndemla, Ramadhani Singano upande wa kulia, katikati
Emmanuel Okwi na Ibrahim Hajibu anakaa nyuma ya Okwi.
Jana alilazimika kutumia mfumo huo huo baada ya
ule wa 4-4-2 kukwama na akamshusha Awadhi Juma nyuma ambapo alicheza mbele
kidogo ya Jonas Mkude, Ndemla akapiga kiungo mchezeshaji, Singano winga ya
kulia, Okwi katikati, nyuma ya Okwi akasimama Ibrahim Hajib.
Baada ya kurudi katika mfumo huo, Mgambo
wakazidiwa kiungo na ndipo mvua ya magoli ikaanza mdogomdogo.
0 comments:
Post a Comment