Tuesday, April 28, 2015

Beki wa kulia wa Arsena Hector Bellerin, anaamini kuwa kitendo chake cha kucheza kama winga wakati akianza kusakatka kabumbu ndiyo kilimsaidia kwa kiasi kikubwa sana kuisaidia timu kupandisha mashambulizi pindi awapo uwanjani.
Beki huyo kinda raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 20, amekuwa kivutio kikubwa sana kwa klabu hiyo hasa baada ya Debuchy kuumia mara mbili mfululizo hali iliyopelekea kumweka kabisa bechi kinda mwenzie Calum Chambers ambaye alisajiliwa kutoka Southampton.
Kwa mara nyingine tena Bellerin alionesha kiwango kikubwa kabisa katika mechi dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita na kumdhibiti vilivyo winga hatari wa Chelsea Eden Hazard kutoleta madhara langoni mwao, ambapo mchezo huo uliisha kwa suluhu.
“Kama watu wengi wanavyofahamu kwamba hapoa awali nilikuwa nikicheza kama winga, ndiyo maana huwa napenda sana kushambulia,” Bellerin aliiambia tovuti ya Arsenal.
“Pengine hicho ndicho kitu bora kabisa nikiwa uwanjani.
“Huwa napenda kuisaidia timu katika upande wote ambao nacheza na nadhani huwa nafanya hivyo pia.
28 Apr 2015

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video