RUVU
Shooting kupitia kwa Msemaji wao, Masau Bwire wamewabeza Yanga wakidai hawana
uwezo wa kutandaza soka maridadi zaidi ya mpira wa kukimbizana kama wanariadha.
Licha ya
kufungwa 7-0 msimu uliopita, Shooting wamedai Yanga hawakuonesha uwezo wa
kucheza soka siku hiyo na kama watu wanabisha basi wakumbuke nini kilitokea
januari 18 mwaka huu ambapo timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya ligi kuu
iliyopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Beki wa
kati wa Ruvu Shooting, George Michael Osei alimkaba ‘Kindava’ mshambuliaji wa
Yanga, Amissi Tambwe na ikafika wakati akambaka kuooni na kumtoa damu mdomoni.
Kutokana
na tendo hilo, Michael alifungiwa mechi tatu baada ya kamera za gazeti la Michezo
la Champion kufichua ukatili huo, lakini Bwire amesema kesho mlinzi huyo kisiki
ataongoza ngome ya ulinzi.
“Yanga
ni watu wa mbio sana, hawamiliki mpira, tatizo lao wanapiga mipira mirefu ya
juu na wanaanza kukimbizana, tuna vijana makini, imara, wenye nguvu na maarifa
mengi ya kucheza mpira, wako tayari kuwadhabiti hao wanariadha” Amesema Bwire
na kusisitiza: “Michael (Geroge Osei) atakuwa miongoni mwa mabeki watakaoongoza
safu ya ulinzi, mabeki wana jukumu la kuhakikisha lango lao linakuwa imara,
namba mbili atamzuia anayemkaba, namba tatu atamzuia anayemkaba, kila mmoja kwa
idara yake atatimiza majukumu yake”.
0 comments:
Post a Comment