Sunday, April 26, 2015

Isihaka (kulia) akiichezea Simba dhidi ya JKT Ruvu

NAHODHA wa Simba, Hassan Suleiman Isihaka afya yake inaendelea kuimarika taratibu kutokana na majeraha aliyopata kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mechi hiyo ilipigwa aprili 18 mwaka huu na Simba kulala kwa magoli 2-0 na Isihaka aliumia dakika ya 23 na kushindwa kuendelea na mchezo.
"Naendelea vizuri, lakini bado siwezi kucheza kwasasa. Tusubiri mechi mbili za mwishoni" Amesema Isihaka.
Isihaka ni kipenzi cha kocha wa Simba Goran Kopunovic na wapenzi wa Simba kutokana na kazi nzuri anayofanya kwenye safu ya ulinzi.
Beki huyo aliyetokea Simba B amekosa mechi mbili dhidi ya Mgambo JKT ambayo Simba walishinda 4-0 na ya jana ambayo Simba walishinda 3-0 dhidi ya Ndanda fc.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video