Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Simba ililazimika kuusitisha kwa muda mkataba wa Kiongera baada ya Mkenya huyo kutonesha majerahab yake ya muda mrefu ya goti na kulazimika kupelekwa India kufanyiwa upasuaji.'
Kiungo mshambuliaji wa KCB, Paul Mungai Kiongera, yuko mbioni kurejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na upasuaji wa goti aliofanyiwa mwishoni mwa mwaka 2014.
Kiongera ambaye yuko kwa mkopo KCB akitokea Simba SC ya Tanzania, bado hayuko fiti kuichezea timu hiyo ya benki msimu huu kwa kuwa bado anaendelea kutibu goti lake lililopasuliwa India mwaka jana.
Kocha wa KCB, Elvis Ayany, ameweka wazi alipohojiwa na mtandao wa futaa.com wa Kenya leo kwamba mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Kenya kwa sasa anafanya mazoezi mepesi na timu na huenda akarejea uwanjani katika muda wiki chache zijazo.
"Kwa sasa yuko fiti kimazoezi, amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wengine wa kikosi chetu, ninaamini katika wiki chache zijazo anaweza kurejea uwanjani, ni mcheza mzuri na sote tunajua ubora wake, kurejea kwake kutakuwa msaada mkubwa kwa timu ukizingatia tunaelekea kumalizika mzunguko wa kwanza wa ligi," amesema.
Timu hiyo ya benki imeyumba msimu huu wa Ligi Kuu ya Kenya; imeshinda mechi moja tu katika mechi nane za KPL.
0 comments:
Post a Comment
Links to this post
Create a Link