Tuesday, April 28, 2015


Kocha wa zamani wa klabu ya mashetani wekundu Manchester United, Sir Alex Ferguson ametanabaisha kuwa ni sababu nyingi tu zinazopelekea Christiano Ronaldo kuwa juu ya Lionel Messi.
 Ferguson alisema hayo alipokuwa akizungumza na John Parrott wakati walipokuwa wakiburudika na mchezo wa pool table ambao pia unajulikana kwa jina la Snooker.
Kocha huyo ambaye mpaka sasa ndiye mwenye mafanikio kwa kiasi kikubwa si tu katika klabu ya Man United bali ligi kuu nchini Uingereza kwa ujumla, alisema hayo katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji nchini Uingereza (BBC) huku akiwa na Parrott na mtangazaji Hazel Irvine wakizungumzia michuano ya Ubingwa wa Dunia ya pool table.
Ferguson mara nyingi huulizwa sana hili swali kuwa ni nani kwa mawazo yake ni mchezaji wa dunia?, lakini kwa mtazamo wake yeye anasema kuwa Ronaldo ni bora zaidi ya Messi.
Ferguson kwa upande wake anaamini kuwa Ronaldo ana ubora zaidi ya Messi kwa sababu ana uwezo wa kucheza ligi yoyote duniani na kufunga kwa kiwango kilekile huku kwa upande wa Messi akisema sio rahisi.

Ferguson anaongeza" Nadhani Ronaldo ni bora, anatumia miguu yote miwili kwa usahihi, ana kasi, yuko vizuri mipira ya kichwa na pia ni jasiri"
"Messi ni mchezaji wa Barcelona tu," alimalizia Ferguson

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video