Je, Javier Hernandez anaweza kukamilisha usajili kutoka Manchester United kwenda Real Madrid majira ya kiangazi mwaka huu?
Chicharito amekuwa na wakati mzuri Santiago Bernabeu baada ya kujionesha kuwa yeye ni noma akiifungia magoli muhimu Real Madrid kwenye mechi mbili.
Wiki iliyopita Chicharito alifunga goli pekee Real Madrid wakitinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya (uefa Champions League) dhidi ya Atletico Madrid na jana jumapili katika mechi ya La Liga, mshambuliaji huyo wa Manchester United aliyepo kwa mkopo Real alikuwa kwenye kiwango cha juu dhidi ya Celta Vigo.
Hernandez alifunga magoli mawili katika ushindi wa 4-2 na kuamusha tena matumaini ya Real Madrid kuipiku Barcelona kwenye mbio za ubingwa.
Katika mechi 8 alizoanza Real Madrid, sasa Chicharito amefunga magoli 6 na kutoa pasi za magoli mbili (2).
Cha zaidi ni kwamba Chicharito ameshika nafasi ya tatu katika uwiano mzuri kufunga magoli kwa dakika katika mechi za La Liga nyuma ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Kwa mujibu wa gazeti la Hispania la AS, Javier Hernandez atawagharimu Real Madrid euro milioni 10 sawa na paundi milioni 7 kama wataamua kumpa usajili wa kudumu majira ya kiangazi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment