MANCHESTER UNITED wanakaribia kukamilisha usajili wa kinda wa PSV, Memphis Depay, kwa mujibu wa gazeti la la leo asubuhi la Sun.
Kijana huyo mwenye miaka 21 mara kadhaa amekuwa akihusishwa kujiunga Old Trafford, lakini Louis van Gaal anakabiliana na changamoto kutoka Liverpool na PSG wanaoiwinda pia saini yake.
Gazeti la The Sun limeripoti kuwa Memphis Depay na wakala wake Kees Ploegsma wamepanda ndege kwenda England kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba ambao nyota huyo atakuwa analipwa paundi laki moja na elfu 30 kwa wiki Manchester United.
Depay amefunga magoli 26 katika mashindano yote akiichezea PSV na mkurugenzi wa timu hiyo, Marcel Brands siku za karibuni amekiri klabu yake kuwa na mpango wa kumuuza Memphis Depay majira ya kiangazi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment