1.
Kuzuia hatari zozote zitokanazo na
adhabu ndogo (set pieces). Tumeona msimu huu kumekuwa na magoli machache
yalotokana na uzembe. Katika msimu huu Barcelona imeweza kuwa na clean sheets
28 katika mechi 51 ambayo ni 54% kulinganisha na misimu mingine ambayo Barca
iliweza kuwa na clean sheets. Rekodi ilioko inaonesha kuwa msimu wa 1986-87
ndio unaokaribia kwa kuwa asilimia 53% (yaani mechi 54 na kuwa na clean sheets
29). Ili kuimarisha uwezo wa kuongeza clean sheets Barcelona inapaswa kuepuka
makosa yasio ya lizima katka eneo la nje ya 18 ‘avoiding unnecessary free
kicks’.
2.
Kucheza kwa umakini, mtu na mtu, (Zonal
marking). Kila mchezaji atoe mchango 120% ili kuhakikisha kunakuwa na team
balance, mabeki wa pembeni wazime mashambulizi ya kushtukiza na kuhakikisha
kuwa kama ni kupanda mbele na kurudi nyuma kutengeneza ‘balance’ uwiano. Jordi
Alba ni mzuri zaidi katika hilo.
3.
Kuendelea kushambulia pasipo kuridhika
na goli1 au mawili. Hapa naona kuna haja ya Enrique kufanyia kazi maana kama ni
kikosi cha kwanza amepata. Kuna mifano kadhaa tumeona mpaka sasa kuwa timu
imekuwa ikicheza kwa kuridhika hasa baada ya kuwa imeongoza. Mfano mzuri ni ile
mechi ya ManCity vs Barcelona na ile ya
Sevila vs Barcelona hivi karibuni ambapo tulishuhudia udhaifu huo.
4.
Kucheza kwa kasi na kupiga pasi zenye
macho. (Moving the ball quickly). Kama kupoza mpira ili kufisha mashambulizi ya
timu pinzani ambapo Xavi Hernandez (‘The living legend’) ni mtaalam katika
hili, ni muhimu sana kufanya hivyo na kuepuka kupoteza mipira kirahisi hasa
katika eneo la katikati na hivyo kuzuia kaunta (mashambulizi ya kustukiza)
ambayo yangeweza kuepukika.
5.
Kutumia nafasi vizuri, (to be clinical
in finishing) na kuwa na ubunifu wa ziada kwa kupiga nje ya box. Kumiliki mpira
ni jambo moja ila kutengenza nafasi na kuitumia ni jambo lingine. Lazima
tukubali kubadilika, timu iburudishe ila itumie nafasi kila inapopatikana. Mara
zote ambapo Neymar na Suarez walipotimiza wajibu wao vema tumeona magoli
yakipatikana.
KILA
LA HERI BARCELONA, Visca el Barca!!
v Itaendelea
wiki ijayo ambapo tutazungumzia ubora na udhaifu wa Bayern. Uchambuzi wa
mchezaji mmoja mmoja (wachezaji wa FC Barcelona na wale FCBayern.) (FCB vs
FCB). Yote ni katika kuona wajibu wa kila mchezaji uwanjani.
0 comments:
Post a Comment