Hans van pluijm akiliongoza jeshi lake kushangilia kwa kuzunguka uwanja pia kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao.
KOCHA mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van der Pluijm ‘Babu’ amesema
kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kumempa faraja kubwa na sasa
anaelekeza nguvu zake kwenye mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho dhidi ya
Etoile du Sahel itayopigwa mwishoni mwa wiki hii nchini Tunisia.
“Siku zote nashangazwa na mashabiki wa Yanga, wananiunga
mkono kwa kiwango cha juu, nafurahia sana maisha ya soka Tanzania, nimechukua
ubingwa wangu wa kwanza baada ya kushindwa mwaka jana, hii ni hatua nzuri
kwangu na sasa naelekeza nguvu zangu kwenye mechi ya kimataifa dhidi ya Etoile”.
Amesema Pluijm na kuongeza: “Tulitoka sare ya 1-1, katika mpira lolote linaweza
kutokea, tutaenda kucheza kwa kushambulia, lazima tupate magoli”.
Aidha, Pluijm amesisitiza kuwa anahitaji kushinda mechi
mbili zijazo za ligi kuu dhidi ya Azam fc na Ndanda fc ili kunogesha zaidi
ubingwa.
“Ligi ni ngumu, timu zinacheza kwa nguvu, nimebakiwa na
mechi mbili, lazima tushinde, hatuna mzaha hata kidogo”. Amesema Pluijm.
Ushindi wa Yanga wa magoli 4-1 waliopata dhidi ya Polisi
Moro umewafanya wafikishe pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Azam wamebakiza mechi tatu, Yanga mbili, lakini wakishinda
zote wanalambalamba watafikisha pointi 54 kutoka 45 walizokusanya mpaka sasa
katika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment