Sunday, April 26, 2015

KIUNGO mkabaji na nahodha msaidizi wa Simba, Jonas Mkude amesema sasa wanajiandaa kwa nguvu zote na mechi ya mwishoni mwa juma lijalo dhidi ya mabingwa watetezi Azam fc itayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba ilishinda magoli 3-0 dhidi ya Ndanda fc wakati Azam waliichapa Stand United magoli 4-0 uwanja wa Azam Complex na kufanya nafasi ya pili iwe ngumu kwa Simba.
Simba wamebakiza mechi mbili kumaliza msimu wakati Azam wana mechi tatu..
Simba wana pointi 41 mpaka sasa wakati Azam wana pointi 45 huku Wanalambalamba wakiwa na mchezo mkononi.
Kama Simba watashinda mechi zao mbili zilizosalia inamaanisha watafikisha pointi 47 na inabidi wawaombee dua mbaya Azam watoe sare moja katika mechi zilizosalia na kufungwa mbili ili waishie pointi 46.
Baada ya mechi ya jana, Mkude alisema: "Mpira ni mchezo wa nafasi, kipindi cha kwanza Ndanda walifanya makosa tukatumia nafasi, kipindi cha pili walijipanga na kufanya vizuri, walijitahidi kutengeneza nafasi lakini tuliwazuia vizuri"
"Tunaangalia mbele, nafasi ya pili ni ngumu, lakini sisi tunachoangalia ni kushinda mechi zote, mambo mengine yatajulikana huko mbele"
Mkude alifunga goli lake la kwanza jana katika ushindi wa  3-0, magoli mengine yalifungwa na Ramadhani Singano na Said Ndemla.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video