Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Klabu ya Yanga imeibuka na madai mazito dhidi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), huku ikitaka watendaji wa bodi hiyo wachunguzwe uwezo wao wa kufikiri na madaraja yao ya elimu.

Aidha, uongozi wa wanajangwani hao, umesema umesikitishwa
na bodi hiyo kuamua kutumia sheria ambazo hazijapata baraka za mkutano
mkuu wa wanachama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumruhusu
mshambuliaji Ibrahim Ajibu wa Simba SC kucheza mechi akiwa na kadi tatu
za njano.
Kanuni za ligi za TFF zinataka mchezaji aliyeoneshwa kadi tatu za njano katika mechi zilizopita, atakosa mechi moja inayofuata, lakini Ajibu alipangwa katika kikosi cha Simba SC kilichoifumua mabao 5-0 Tanzania Priasons FC Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumamosi.
Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, amesema jijini hapa leo mchana kuwa uongozi wa Simban SC uliwasilisha barua TPLB kumwombea Ajibu acheze katika mechi mbili dhidi ya Prisons na Yanga SC, kisha asiche dhidi ya Mtibwa Sugar SC kutumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano.
Huku akionesha barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Ofisa Mtendaji wa bodi hiyo, Fatma Shibo, Muro amedai TPLB imemruhusu mkali huyo wa mabao kucheza dhidi ya Prisons FC na Yanga FC kinyume cha kanuni na taratibu zilizopo.
"Inatushangaza, kwa nini watumie sheria ambazo zimependekezwa na bado hazijapitishwa na mkutano mkuu wa TFF kwa ajili ya kuanza kutumika? Wameanza kutumia kanuni ambazo hazijapata baraka za mkutano mkuu wa wanachama wa TFF," amesema Muro.
Amesema mchezaji wao, Mrwanda mweny asili ya DRC, Mbuyu Twite alikosa mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City FC mjini Mbeya ili kutumikia kadi tatu za njano, lakini Simba SC haijafuata utaratibu huo.
Mtangazaji huyo wa zamani wa ITV na TBC, amesema nakala za barua hiyo zimepelekwa kwa Mwenyekiti wa bodi hiyo, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Kamati ya Waamuzi pamoja na timu za Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar.
"Kuendelea kufanya vitendo kama hivi, mpira wa Tanzania utaendelea kudidimia badala ya kwenda mbele," amesema zaidi Muro huku akihoji ni vipi kiongozi mmoja wa klabu anashika vyeo vitatu, kimoja cha klabu na viwili vya ndani ya shirikisho akimlenga Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo.

0 comments:
Post a Comment