Klabu ya Yanga imepinga maamuzi ya Bodi ya Ligi ya Vodacom kwa
kuahirisha mchezo wao wa kesho Jumatano waliyokuwa wacheze dhidi ya klabu ya maafande wa JKT Ruvu
na badala yake wameusogeza mchezo huo hadi Machi 11 huku siku tatu baada
ya mchezo huo Machi 14 wakikabiliwa na mchezo wa kimataifa wa Kombe la
Shirikisho Afrika CAF, dhidi ya FC Platinum ya nchini Zimbabwe.
Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro ameiambia Mpenja,
kuwa hawakubaliani na maamuzi ya Bodi ya Ligi ya kuwabadilishia ratiba
ghafla huku wao wakiingia kambini kujiandaa na mchezo wa kesho na JKT
Ruvu na siyo ule wa Machi nane dhidi ya watani zao wa jadi Simba.
“Kwa mabadiliko haya ya ratiba Bodi ya ligi imeshindwa kuthamini
ushiriki wetu katika michuano ya kimataifa kama wawakilishi pekee wa
Tanzania haiwezekani kuisogeza mbele mechi yetu ya kesho hadi Machi 11,
wakati baada ya mchezo huo siku mbili zijazo Machi 14 tunatakiwa
tucheze na FC Platinum ya Zimbabwe mchezo wa kimataifa,”alisema Muro.
Muro alisema haoni sababu ya mchezo wao wa kesho
kusogezwa mbele kwani walitoka Botswana na kuingia kambini kwa ajili
ya mchezo huo na siyo ule wa Simba kwa sababu hawana hofu na timu hiyo
ya bonanza iliyopoteza ushindani na kubaki na utani pekee.
“Yanga haiwezi kuwa na upinzani na timu kama Simba ambayo haina
tofauti na timu za bonanza wapinzani wa Yanga kwa sasa ni TP Mazembe,
Azam na Kaizer Chief s,” alisema Muro.
0 comments:
Post a Comment