Wednesday, March 25, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Yanga SC imezidi kuikomalia klabu ya Simba baada ya leo kutishia kutinga FIFA endapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lisipoipoka pointi klabu hiyo Msimbazi kutokana na kumchezesha mshambuliaji Ibrahim Ajibu akiwa na kadi tatu nza njano.

Simba SC ilimpanga Ajibu katika kikosi chake kilichoshinda 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Februari 28 na 1-0 dhidi ya Yanga SC kwenye uwanja huo Machi 8 ilhali alikuwa na kadi tatu za njano (alikuwa na kadi nne za njano katika mechi yao dhidi ya Yanga SC) ikitumia kanuni mpya ya kadi za njano iliyopitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake cha Februari 8, mwaka huu.

Hata hivyo, kanuni hiyo inayoiruhusu klabu kumwombea ruhusa mchezaji mwenye kadi tatu za njano kuchagua mechi moja kati ya tatu zinazofuata kutumikia adhabu, ilisambazwa na TFF kwa makatibu wa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara Machi 14, mwaka huu, suala ambalo limewakera Yanga SC kwa vile tayari watani wao wa jadi, Simba SC walikuwa wameshaanza kuitumia kanuni hiyo kabla ya waraka wa mabadiliko ya kanuni husika kusambazwa.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga inayoongozwa na Jerry Muro, imeeleza kuwa klabu hiyo ya Jangwani imetoa masharti manne kwa TFF kuyatekeleza vinginevyo watatinga FIFA kueleza 'madudu' yanayofanywa na TFF.

"Timu yoyote ambayo imetumia kanuni hii, inyang'anywe pointi za mechi zake katika mchezo husika," linasomeka sharti la pili la Yanga SC kwa TFF.

"Viongozi wote waliohusika katika kuleta mswaada na kuamua kuitumia kanuni kabla ya wakati, wachukuliwe hatua kali na TFF maana wameharibu na kushusha hadhi ya shirikisho katika kuongoza mpira wa miguu nchini.

"Mapendekezo ambayo Yanga SC iliyatoa katika barua yake ya tarehe 05 Machi 2015 yafanyiwe kazi (kuipoka Simba pointi tatu dhidi ya Prisons, kuwawajibisha watendaji wa TFF, Simba SC na Bodi ya Ligi Kuu nchini -TPLB).

"Endapo mambo haya hayatafanyiwa kazi, basi Yanga itawasilisha malalamiko yake FIFA ili kuonyesha upungufu huu," inaeleza zaidi taarifa hiyo.

Kabla ya kutoa masharti hayo, taarifa hiyo imeeleza kuwa Yanga SC inapinga mabadiliko ya kanuni ya 37(3) kuhusu kadi tatu za njano kwa vile kanuni mpya ya TFF haiwiani na kanuni za mashindano za nchini nyingine yakiwamo mashirikisho ya kiimataifa kuanzia CECAFA, CAF hadi FIFA.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video