Saturday, March 21, 2015


KOCHA msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' amesema mwisho wa Mgambo kuzikazia timu kubwa, Simba, Yanga katika uwanja wa Mkwakwani umefika.
"Mgambo ni wagumu kufungika Mkwakwani, lakini kila jambo lina mwisho wake. Wametoka kuwafunga Simba 2-0, sisi tumejiandaa kufuta rekodi hiyo na wachezaji wetu wanalifahamu hilo, mashabiki wategemee soka safi". Amesema Mkwasa.
Mgambo na Yanga zinachuana leo jioni katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga kuanzia majira ya saa 10:00.
Jana jioni Yanga walifanya mazoezi uwanja wa Mkwakwani, lakini mvua ilikatisha mazoezi hayo.
Mechi hii itarushwa moja kwa moja na Azam TWO ya Azam TV.
Mechi nyingine itashuhudiwa huko Nangwanda Sijaona ambapo Ndanda FC itachuana na JKT Ruvu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video