LIGI kuu soka Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho kwa mechi moja ya kiporo kupigwa uwanja wa Taifa jijini Dra es salaam.
Mabingwa mara 24 wa Tanzania, Dar Young Africans watachuana na maafande wa jeshi la kujenga Taifa, JKT Ruvu Stars.
Kiporo hicho kilipangwa kufanyika machi 11 mwaka huu, lakini Yanga waligoma wakati ule wanakwenda Zambabwe kucheza mechi ya marudiano dhidi ya BDF XI.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wapo tayari kwa mechi na wamefanya mazoezi leo asubuhi tayari kwa kuvuna pointi tatu muhimu.
Yanga wanangoza ligi kwa kujikusanyia pointi 37 kileleni baada ya kushuka dimbani mara 18, wakifuatiwa na Azam fc wenye pointi 36 nafasi ya pili wakicheza mechi sawa na Yanga.
Mwishoni mwa wiki, Azam watapiga kiporo chao na Mgambo JKT uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.
0 comments:
Post a Comment