LIGI Kuu Tanzania bara inaendelea kutimua vumbi leo Jumatano kwa viwanja vitatu kuwaka moto.
Uwanja wa Taifa jijini Yanga watawakaribisha Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera, mchezo utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Yanga wanatarajia kulipa kisasi kwani mechi ya kwanza walifungwa bao 1-0 uwanja wa Kaitaba, goli pekee la Paul Ngwai.
Aidha Yanga wataingia na nguvu baada ya kuitandika FC Platinum ya Zimbabwe mabao 5-1 katika mechi kwanza ya raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini wana machungu ya kufungwa 1-0 na Simba katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa machi 8 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Jijini Tanga maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Simba SC katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani, huku jijini Mbeya wenyeji Mbeya City watawakaribisha timu ya ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga kwenye uwanja wa Sokoine.
0 comments:
Post a Comment