Na Bertha Lumala, Tanga
Nyota 13 wa Azam FC wameondoka katika klabu hiyo ya Chamazi jijini Dar es Salaam kwenda kutekeleza majukumu mengine.
Jaffar Idd Mganga, msemaji wa Azam FC, amesema wachezaji wao wamepewa mapumziko hadi Alhamisi kupisha mechi ya timu za taifa zilizopo katika Kalenda ya Matukio ya FIFA.
"Wachezaji wetu 10 wameitwa Taifa Stars, (Didier) Kavumbagu na (Brian) Majwega wamerudi nchini kwao kuzitumikia timu zao za taifa wakati (Serge) Wawa amepewa ruhusa maalum wa kurejea nyumbani kwao, lakini ataingia kambini Alhamisi kujiandaa kwa mechi yetu inayofuata dhidi ya Mbeya City FC," amesema zaidi Maganga.
Kavumbagu, Majwega na Wawa wamekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha wanalambalamba tangu wajiunge nacho msimu huu.
Wawa ndiye beki wa kati tegemeo katika kikosi cha kocha mkuu Mganda George Nsimbe huku Kavumbagu akiwa kina wa mabao Azam FC na Ligi Kuu Bara kwa sasa.
Winga Brian Majwega, ambaye alisajiliwa dirisha dogo msimu huu akitokea kwa mabingwa wa Uganda, KCCA FC, ndiye anayeonekana kuwa winga fundi kuzidi wote Ligi Kuu Bara akiongoza kwa kupika mabao Azam FC tangu atue licha ya kwamba hajawahi kufunga bao hata moja.
0 comments:
Post a Comment