Yanga walipochuana na Mgambo JKT msimu uliopita
LIGI kuu Tanzania bara kuendelea kesho kwa mechi mbili kupigwa miji miwili nchini.
Maafande wa jeshi la kujenga Taifa, Mgambo JKT wataikaribisha Dar Young Africans katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Mgambo walioifunga Simba jumatano ya wiki hii mabao 2-0 watakutana na Yanga iliyofungwa 2-1 katika uwanja huo msimu uliopita.
Tayari Yanga ipo jijini Tanga toka jana na asubuhi hii wamefanya mazoezi uwanja wa Mkwakwani.
Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' amesema: "Tutakabiliana na Mgambo ambao ni wagumu kufungwa Mkwakwani, lakini kila jambo lina mwisho wake".
Mechi nyingine itashuhudiwa uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara ambapo wenyeji Ndanda fc watachuana na maafande wa JKT Ruvu Stars Stars.
Kocha wa Ndanda fc, Meja mstaafu Abdul Mingange amesema baada ya kufungwa na Azam fc 1-0 mwanzoni mwa wiki hii, lazima JKT wakae kesho.
Ligi hiyo itendelea jumapili ambapo Simba watakuwa wageni wa Ruvu Shootings uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Tanzania Prisons watachuana na Polisi Morogoro uwanja wa CCM Sokoine Mbeya.
Kibarua kingine kikali kitakuwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Coastal wakiwakaribisha Azam fc.
0 comments:
Post a Comment