Baada ya kikosi cha Manchester United kutolewa katika michuano ya kombe la FA kwa kipigo cha 2-1 kutoka kwa Arsenal jumatatu iliyopita, kocha wa klabu hiyo Louis Van Gaal amesema nguvu zake zote anazielekeza katika ligi kuu ili aweze kupata nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa msimu ujao.
Kocha huyo amesema kikosi chake hakina uwezo wa kushinda kombe lolote msimu huu baada ya kutolewa katika kombe la FA hivyo wakimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu itakuwa ni kama wameshinda kombe kutokana na ushindani uliopo kunako ligi hiyo "Nilipenda tucheze nusu fainali katika kombe la FA lakini tumetolewa, hivyo nafasi iliyobaki ni kuwania kumaliza katika nafasi nne za juu na hii itakuwa kama tumeshinda kombe msimu huu " alisema Van Gaal.
Manchester United imeibuka na ushindi wa 3-0 katika mechi ya jana waliyocheza dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye dimba la Old Trafford na mechi ijayo wanakibarua kizito dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield
0 comments:
Post a Comment