KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal ameweka wazi kuwa hataendelea na kazi ya kufundisha soka baada ya kumaliza kazi Old Trafford.
Van Gaal na vijana wake watakabiliana na Liverpool jumapili kujaribu kutafuta ushindi ili kujiweka nafasi nzuri katika msimamo wa ligi kuu England.
Mholanzi huyo amekiri kuwa jaribio lake la kurudisha ufalme wa United ndio itakuwa kazi yake ya mwisho kwenye soka.
"Van Gaal amewaambia The Telegraph: "Nimezeeka. Kukweli hii ni kazi yangu ya mwisho.
"Nahitaji kuwatunza wanangu, wajukuu zangu, pia lakini pia mke wangu. Wanastahili sasa. Kwa mfano sikuwepo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mjukuu wangu. Sipendi kabisa".
0 comments:
Post a Comment