ANTONIO Valencia ameiomba radhi Manchester United na mashabiki wake kufuatia kufanya makosa yaliyoifanya klabu hiyo itolewe kombe la FA na Arsenal kwenye mechi ya robo fainali iliyochezwa jumatatu wiki hii.
Kutupwa nje kwa United kuliondoa rasmi matumaini ya ya vijana wa Louis van Gaal kuvaa medali yoyote msimu huu na Valencia amechangia janga hilo kwa kiwango kikubwa.
Kiungo huyo wa pembeni alimkaba kidhaifu Alex Oxlade-Chamberlin aliyetengeneza nafasi ya kufunga kwa Nacho Monreal na hatimaye akapiga pasi dhaifu ya nyuma iliyosababisha Danny Welbeck afunge goli la pili na la ushindi kwa Arsenal.
Ujumbe wake wa kuomba radhi huu hapa:
0 comments:
Post a Comment