Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer)
inatarajiwa kuodoka siku ya alhamisi kuelekea jijini Cairo nchini Misri kwa
ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa
soka la ufukweni utakaofanyika siku ya jumapili.
Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano
dhidi ya Misri utakaofanyika siku ya jumapili jijini Cairo ili kufuzu kwa
fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli
kufuatia kupoteza mchezo wake awali uliofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam
mwishoni mwa wiki.
Msafara wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na shirika la
ndege la Ethiopia, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri
Mgoyi, kocha mkuu John Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja
Deogratius Baltazar na daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.
Wachezaji ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus
Kessy, Samwel Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima,
Mwalimu Akida Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby
Abdallah.
0 comments:
Post a Comment