Tuesday, March 10, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Ule mgomo wa Yanga SC kuingiza timu uwanjani kesho umeungwa mkono na TFF baada ya shirikisho hilo la soka nchini kufuta mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizokuwa zichezwe kesho.

Wiki iliyopita Yanga SC kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Jerry Muro, ilitangaza kuwa haitaingiza timu kwenye Uwanja wa Taifa kesho Jumatano kucheza dhidi ya JKT Ruvu Stars kwa kuwa ina mechi ngumu ya kimataifa dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe kwenye uwanja huo huo  mwishoni mwa wiki.

Jana TFF kupitia kwa msemaji wake, Baraka Kizuguto ilitoa taarifa ikionesha kesho Jumatano kutakuwa na mechi mbili za JKT Ruvu Stars dhidi ya Yanga SC (Taifa) na Mgambo JKT dhidi ya Azam FC (Mkwakwani).

Hata hivyo, Jemedaari Said, Meneja wa Azam FC, amesema wametumia taarifa na TFF leo asubuhi kwamba mechi yao dhidi ya Mgambo JKT kesho haitachezwa hadi pale itakapopangiwa tarehe baadaye.

"Tulikuwa tufane mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya safari ya kwenda Tanga kucheza dhidi ya Mgambo, lakini tumepata taarifa kutoka TFF kwamba mechi hiyo haipo kesho," amesema Jemedari.

Aidha, mmoja wa watendaji wakuu wa TFF amekaririwa na moja ya vituo vya redio jijini hapa leo asubuhi akieleza kuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameagiza mechi zote za KESHO Jumatano ziahirishwe.

Hata hivyo, haijaelezwa ni kwa nini kiongozi huyo wa juu ameamua kutoa tamko hilo huku mshauri wake, Peregenus Rutayunga akikiambia kituo hicho cha redio kwamba Kamati ya Utendaji ina mamlaka ya kuingilia muda wowote utendaji wa vyombo vyake visivyo wa kisheria (judicial organs).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video