Saturday, March 28, 2015



Katika kuthibitisha ina nia njema na ya dhati ya kuinua soka la Tanzania, kabla ya kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Septemba 20, Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ilitangaza neema kwa wachezaji wanaojituma.

    Uongozi wa kampuni hiyo ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa ligi, uliahidi kutoa zawadi ya Sh. milioni moja na kombe kwa mchezaji anayeng'ara kwa kila mwezi wa kila mwezi wa ligi hiyo, yaani tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa VPL

     Hata hivyo, nia hiyo njema ya Vodacom Tanzania kuhakikisha soka la Bara linakua, imekuwa ikididimizwa na kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuachia utaratibu mbovu wa kumpata Mchezaji Bora wa Mwezi wa VPL uendelee.

       Kwa wanaofuatilia kwa kina VPL msimu huu, watakubaliana na mimi kwamba tangu tuzo hizi zianze kutolewa Septemba mwaka jana, hakuna hata mchezaji mmoja aliyetwaa tuzo hiyo kihalali kama taratibu sahihi katika kumpata Mchezaji Bora wa Mwezi zingelifuatwa.

       Wiki iliyopita TFF ilitangaza kuwa kiungo Godfrey Wambura wa Coastal Union amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Februari wa VPL akiwabwaga Simon Msuva wa Yanga, Gideon Benson wa Ndanda FC na Abasirim Chidiebere wa Stand United ambaye ndiye alistahili tuzo hiyo.

      Kwa mujibu wa Baraka Kizuguto, Ofisa Habari wa TFF, Wambura amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya jopo la makocha linalofanya majumuisho ya wachezaji bora wa kila mchezo.

      Wambura anakuwa mchezaji wa pili wa Coastal Union kutwaa tuzo hiyo isivyo halali tangu ianzishwe msimu huu baada ya kiungo mkabaji Joseph Mahundi wa mabingwa hao wa 1988 wa Tanzania Bara, kuibuka Mchezaji Bora wa VPL Mwezi Desemba.

         Mchezaji Bora wa Mwezi, angalizo kwa jopo la makocha la TFF, anapaswa kuwa yule ambaye alitoa mchango mkubwa uwanjani katika kuipa timu yake mafanikio ambayo ama hayakufikiwa na timu nyingine, au hayakupitwa na washindani wao katika kipindi hicho.

         Chidiebere ndiye aliyepaswa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Februari kutokana na mchango wake mkubwa katika kikosi cha Stand United.

         Mwezi uliopita timu hiyo ya usukumani mjini Shinyanga, ilicheza mechi tano ikifungwa 2-1 ugenini dhidi ya Ruvu Shooting, ikatoka sare ya bao moja (1-1) ugenini dhidi ya Ndanda FC kabla ya kushinda nyumbani 4-1 dhidi ya Mgambo Shooting, 1-0 dhidi ya Simba na 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

          Katika mechi hizo ilizokusanya pointi 10, Chidiebere raia wa Nigeria, alifunga mabao sita na kuwa mchezaji pekee wa VPL aliyefunga mabao mengi zaidi mwezi huo huku Stand ikikwea kutoka nafasi ya 12 hadi nafasi ya saba katika msimamo wa ligi.

          Yanga ndiyo timu iliyokusanya pointi nyingi zaidi Februari (pointi 13) ikitoka suluhu dhidi ya Ndanda FC na kushinda 1-0 dhidi ya Coastal Union, 2-0 Mtibwa Sugar, 3-0 Tanzania Prisons na 3-1 Mbeya City.

          Jopo la makocha la TFF lingelimchagua mmoja wa wachezaji wa Yanga kutwaa tuzo hiyo, lingelieleweka kwa umma lakini mawinga wake Mrisho Ngasa na Msuva waliong'ara katika kikosi cha wanajangwani mwezi huo, hawakuifikia idadi ya mabao ya Chidiebere. Walifunga mabao matatu kila mmoja katika mechi zote tano.

          Licha ya Yanga kung'ara mwezi uliopita, Msuva ndiye mchezaji pekee wa timu hiyo ya Jangwani aliyeingia katika mchuano wa kumsaka Mchezaji Bora wa Februari akiwa amefunga nusu ya mabao ya Chidiebere ndani ya mwezi huo.

         Yanga ilifuatwa na Stand kwa kufanya vizuri mwezi uliopita ikikusanya pointi 10 ikifuatwa na na Kagera Sugar (9), Ndanda FC (8), Simba (7), Ruvu Shooting, Azam FC na Coastal (6), Mbeya City na Mgambo (3), Prisons (2), Mtibwa, JKT Ruvu na Polisi Moro wakiambulia pointi moja tu kila mmoja.

          Kikosi cha kocha mkuu Mkenya James Nandwa cha Coastal Union kilikusanya pointi sita mwezi uliopita kikifungwa 1-0 nyumbani dhidi ya Yanga, suluhu dhidi ya Simba na Mbeya City (Tanga), kikapoteza 0-1 dhidi ya  Ndanda FC (Mtwara) kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Mgambo (Tanga).

         Katika mechi hizo tano Wambura (aliyepewa tuzo ya Chidiebere) hakufunga kwani bao lao pekee la mwezi lilifungwa na Lutimba Yayo.

Mchezaji Bora Januari
Mshambuliaji Said Bahanunzi anayeichezea Polisi Moro kwa mkopo akitokea Yanga, alichaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari wa VPL.

JKT Ruvu ndiyo timu iliyokusanya pointi nyingi zaidi Januari (pointi 8) ikifuatwa na Azam, Ndanda na Mbeya City (7), Polisi Moro na Simba (6), Ruvu Shooting, Coastal na Mgambo (5), Yanga (4), Prisons (3), Mtibwa na Kagera (2) kisha Stand ikafunga mlango kwa kuambulia pointi moja tu.

Ndani ya mwezi huo, mshambuliaji Samwel Kamuntu kwa mtazamo wangu ndiye aliyestahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa VPL, alifunga mabao manne huku Bahanunzi aliyetuzwa tuzo hiyo akifunga mabao mawili.

Siyo hilo tu, ndani ya mwezi huo JKT Ruvu ilipaa kutoka nafasi ya nne katika msimamo wa VPL hadi nafasi ya kwanza huku Polisi ikiishia nafasi ya tatu.

Mabao ya Kamuntu yaliipa timu ya kocha mkuu Felix Minziro pointi nane ikishinda 0-1 dhidi ya Coastal (Tanga), 2-1 dhidi ya Stand (Dar), sare ya bao moja (1-1) dhidi ya Mtibwa (Dar) na 1-1 dhidi ya Mgambo (Dar) wakati mabao ya Bahanunzi yaliifanya Polisi ikusanye pointi nne, hivyo ni wazi Kamuntu ndiye aliyestahili tuzo na si Bahanunzi aliyetangazwa na TFF.

Mchezaji Bora Desemba
Kiungo mkabaji wa Coastal Union, Mahundi alitangazwa na TFF kuwa ndiye mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Desemba.

Hata hivyo, timu zote 14 za VPL msimu huu zilicheza mechi moja tu katika mwezi wa mwisho wa mwaka 2014.

Ligi ilisimamishwa kwa wiki saba baada ya mechi saba, hivyo kuufanya mwezi Desemba kuwa na raundi moja tu ya ligi na kwa mtazamo wangu, hapakupaswa kuwa na mshindi kwa sababu hapakuwa na mfululizo wa matukio kwa ajili ya kufanyiwa tathmini.

Lakini, hata kama akili ya TFF iliona kasma ya fedha za Vodacom kwa kipengele hicho haikustahili kuachwa kutumika, Mchezaji Bora wa Desemba hakupaswa kutoka Coastal kwa sababu:

Kwanza palikuwa na timu nne zilizokuwa na mafanikio makubwa kuliko ya Wagosi wa Kaya kwenye raundi hiyo, na kwa kigezo hicho pekee, ama mfungaji wa bao la Kagera Sugar lililoilaza Simba 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Dsemba 26, ama mpishi wa goli hilo au mchezaji mwingine yeyote wa Kagera aliyefanikisha kuizua Simba japo kusawazisha, alistahili tuzo hiyo.

Kama si mmoja kati ya hao, ninafikiri yeyote kati ya waliosaidia kuzipa ushindi timu za Ruvu Shooting, Polisi Morogoro na Mbeya City (timu nyingine tatu zilizoshinda Desemba) ndiye aliyestahili na si Mahundi aliyetangazwa na TFF.

Mchezaji Bora Novemba
Mshambuliaji Rashid Mandawa ndiye aliyetangazwa na TFF kuwa mkali wa mwezi Novemba VPL.

Katika mwezi huo kulikuwa na raundi mbili (raundi ya 6 na 7) na Polisi Moro ndiyo timu pekee ilyofanikiwa kuchukua pointi zote sita kwa kushinda 2-1 ugenini dhidi ya JKT Ruvu (Dar) na 1-0 dhidi ya Prisons (Morogoro) ikifuatwa na Kagera, Stand na Simba zilizokusanya pointi nne kila moja, Coastal, JKT Ruvu, Ndanda, Mgambo na Azam (3), Mtibwa (2) Prisons (1) huku Mbeya City na Ruvu Shooting zikitoka kapa.

Mandawa alifunga bao moja katika mechi zote mbili. Alifunga bao la kusawazisha katika mechi ya sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwa siku mbili kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Novemab 8-9.

Binafsi ninafikiri mshambuliaji Danny Mrwanda (sasa mchezaji wa Yanga) alistahili tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL Novemba kutokana na mchango wake mkubwa ulioipa Polisi Moro pointi sita kwa kufunga mabao yote matatu (2-1 dhidi ya JKT na 1-0 dhidi ya Prisons).

Kama jopo la makocha la TFF halikuridhika na kiwango cha Mrwanda, basi mpishi wa mabao yake ama mchezaji yeyote aliyekuwa na mchango mkubwa kwa kikosi cha Polisi alistahili maana timu hiyo ilizifunika timu zote mwezi huo.

Mchezaji Bora Oktoba
Kulikuwa na raundi tatu za VPL Oktoba na hakuna timu iliyofanikiwa kupata pointi zote tisa. Timu zilizong'ara ni Coastal, Ruvu Shooting, Mtibwa na Yanga, zote zikikusanya pointi saba zikifuatwa na JKT Ruvu (6), Azam (4), Mgambo, Kagera na Simba (3), Polisi, Prisons na Stand (2) Mbeya City (1) huku Ndanda ikimaliza mwezi bila pointi.

TFF ilimtangaza kiungo mshambuliaji Salum Abubakar 'Sure Boy' kuwa ndiye aliyeng'ara kuliko wachezaji wote wakati timu yake ikishindwa hata kukusanya nusu ya pointi zote tisa za Oktoba.

Mmoja kati ya washambuliaji, viungo ama mabeki wa moja kati ya timu za Coastal, Mtibwa, Ruvu Shooting na Yanga ndiye aliyestahili tuzo hiyo kutokana na timu hizo kufanya vizuri mwezi huo.

Katika mechi zote tatu, Coastal ilifunga mabao matano na kufungwa mawili (5-2), Ruvu Shooting 4-1, Mtibwa 3-0, Yanga 5-1 wakati Azam FC ilifunga bao moja na kufungwa moja pia.
 
Mchezaji Bora Septemba
Kiungo Antony Matogolo wa Mbeya City (sasa yuko kwa mkopo Panone FC ya Kilimanjaro) ndiye aliyekuwa wa kwanza kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa VPL alipotangazwa na TFF kuwa ndiye aliyeng'ara Septemba.

Kama ilivyokuwa Novemba, Septemba kulikuwa na raundi mbili tu za ligi. Azam FC na Mtibwa Sugar ndizo zilizofanya kweli mwezi huo kwa kukusanya pointi zote sita, zote zikifunga mabao 5 na kuruhusu kufungwa bao moja.

Timu hizo zilifuatwa na Mbeya City iliyokusanya pointi nne ikifunga bao moja tu, tena la penalti katika mechi zote mbili dhidi ya JKT Ruvu na Coastal.

Mgambo, Yanga, Stand, Ndanda, Kagera na Prisons zilikusanya pointi tatu kila moja zikifuatwa na Simba (2) wakati Polisi, JKT Ruvu na Coastal ziliambulia pointi moja huku Ruvu Shooting ikimaliza mwezi bila pointi.

Kwa takwimu hizi, ni wazi kwamba Mchezaji Bora wa VPL Septemba alipaswa kutoka Mtibwa au Azam FC na si Matogolo wa Mbeya City kwa sababu timu yake ilizidiwa kimafanikio na timu hizo mbili zilizokuwa kileleni mwa msimamo mwezi huo.

Ninaishauri Kamati ya Utendaji ya TFF kukaa na jopo lao la makocha na kuangalia upya vigezo wanavyovitumia kumpata Mchezaji Bora wa Mwezi wa VPL kwa vile utaratibu wa sasa hauwiana na utaratibu unaotumika sehemu mbalimbali duniani.

Wachezaji Bora wa VPL
Jina    Timu     Mwezi
Antony Matogolo    Mbeya City    Septemba
Salum Abubakar    Azam FC    Oktoba
Rashid Mandawa    Kagera Sugar    Novemba
Joseph Mahundi    Coastal Union    Desemba
Said Bahanunzi    Polisi Morogoro    Januari
Godfrey Wambura    Coastal Union    Febr

Uchambuzi huu umeandikwa na Sanula Athanas, mwandishi wa michezo mwandamizi wa gazeti la Nipashe   

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video