Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya England Daniel Sturridge ametolewa katika kikosi cha timu ya taifa baada ya kufanyiwa uchunguzi hapo jana na kugundulika anamaumivu makali juu ya paja.
Mchezaji huyo aliwasili jana katika uwanja wa St.George Park ambapo kikosi hicho cha Roy Hodson kinafanyia mazoezi ili kuonana na madaktari wa timu hiyo ambao baada ya kumfanyia uchunguzi waliona majeraha hayo ambayo aliyapata katika mechi ya juzi waliyofungwa na Manchester United.
Sturridge,25, amekuwa mchezaji wa pili wa Liverpool kutolewa katika kikosi hicho baada ya hapo awali Adam Lallama kutolewa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo wa Tottenham Hotspurs Ryan Mason ambaye hajawahi kuichezea England hata mechi moja.
Hivyo wachezaji hao watakosa mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa Ulaya 2016 dhidi Lithuania itakayopigwa ijumaa hii kwenye uwanja wa Wembley na ile ya kirafiki dhidi ya Italia kule Turin jumanne ijayo.
Aidha hili ni pigo kwa kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ambaye alimkosa Daniel Sturridge kwa muda mrefu mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha aliyoyapata wakati akiwa na timu ya taifa.
0 comments:
Post a Comment