Sunday, March 29, 2015

Dar es Salaam.Baba mzazi na kocha wa bondia Mohamed Matumla Junior, Rashid Matumla ‘Snake Man’ amesikitishwa na ushindi wa pointi aliopata mwanaye dhidi ya Mchina, Wang Xia Hua.
Matumla, bingwa wa zamani wa dunia wa WBU alisema, mwanaye alistahili kumaliza pambano mapema kabla ya raundi kumalizika kwani mpinzani wake hakuonyesha kiwango.
“Mudy (Matumla Jr.) alicheza vizuri na kama siyo uvumilivu wa Mchina, tungemaliza pambano raundi za mwanzo, tungechukua ubingwa kwa KO, uvumilivu ulimsaidia Hua,” alisema Matumla.
Matumla Jr aliibuka bingwa wa dunia wa WBF kwenye uzani wa bantam kwa ushindi wa majaji 3-0 kwa pointi 98-92, 99-92 na 97-92 kwenye pambano hilo.Akicheza mbele ya maelfu ya mashabiki kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Matumla alitulia na kufanya mashambulizi kadhaa kwa mpinzani wake kuanzia raundi ya pili hadi ya nane.
Hali hiyo iliamsha shangwe kwa mashabiki wake huku wakizima kabisa kelele za raia wachache wa China waliojitokeza kwa wingi ukumbini hapo kumunga mkono Wang ambaye aliwanyanyua mashabiki hao raundi ya kwanza na baada ya raundi hiyo kumalizika alifanya mashambulizi machache ya kushtukiza kwa Matumla Jr. ambaye muda wote alikuwa akishambulia.
Hata hivyo, kama Matumla angekuwa makini angemaliza pambano hilo raundi ya saba baada ya Wang kulegea na kuonekana kukata pumzi, lakini bondia huyo chipukizi hakutumia udhaifu huo wa mpinzani wake ambaye alionyesha uvumilivu licha ya kupasuliwa kwa konde la Matumla juu ya jicho la kushoto.
“Pambano lilikuwa gumu kwani mpinzani wangu alionyesha kiwango, nashukuru nimeshinda na kutwaa ubingwa huu,” alisema Matumla akiwa ameambatana na babu yake, Issa Matumla.
Kwa ushindi huo, Matumla Jr anasubiri ripoti ya Shirikisho la Ngumi la Dunia la WBF ambalo rais wake, Howard Goldberg aliyefuatana na bingwa wa zamani wa dunia kwenye uzito wa juu, Francois Botha ili kupata fursa ya kuzichapa kwenye pambano la nguli wa dunia, Floyd Mayweather na Manny Pacquiao, Mei 2.
Source: Mwananchi

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video