Hajji Manara (kulia) akiongea na waandishi wa habari, kushoto ni katibu mkuu wa Simba SC, Stephen Ally
AFISA habari mpya wa klabu ya Simba, Hajji Manara ametambulishwa rasmi na uongozi wa klabu hiyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi Kariaokoo, Dar es salaam.
Hajji anarithi kiti cha Humphrey Nyasio aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.
Mara baada ya kutambulishwa na katibu mkuu wa Simba, Stephen Ally, Hajji, mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Sunday Manara ameishukuru klabu yake kumteua yeye tena akiwa mlemavu wa ngozi 'Albino' , huku wenzake wanaendelea kuchinjwa nchini na akasema Simba ndio wapiganaji wa kweli.
Manara baada ya kutangazwa nayeye ametangaza utaratibu mpya wa idara yake akisema kila ijumaa watakuwa na mkutano na waandishi wa habari, lakini kocha wao atazungumza na waandishi mara moja kwa mwezi na yeye hatakuwa anaongea mambo ya ufundi.
Katibu mkuu wa Simba, Stephen Ally (kushoto) akifafanua suala la Danny Sserunkuma
Katika mkutano huo, katibu mkuu, Stephen amefafanua suala la mshambuliaji wao, raia wa Uganda, Danny Sserunkuma kuwa aliondoka kwa ruhusa yao akiuguliwa na mkewe Kenya na leo anarejea.
Katibu huyo amesema sio kweli kwamba aliondoka kwa kuhusishwa katika ushirikina taarifa ambazo hata mwenyewe Sserunkuma alizikanusha.
0 comments:
Post a Comment