TOKA Mgambo JKT ipande ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013 imekutana na Simba mara 4.
Imeshinda mara 1, imefungwa mara mbili na kutoa suluhu mara 1.
Oktoba 21 mwaka 2012 uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Mgambo JKT ilitoka suluhu (0-0) na Simba. Mechi ya marudiano uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Mei 8, 2013, Simba ikashinda 1-0.
Msimu uliofuata (2013/2014) Simba chini ya Abdallah Kibadeni, septemba 18 mwaka 2013 iliishindilia Mgambo JKT 6-0 Uwanja wa Taifa Dar es salaam. Mechi ya marudiano Mkwakwani Tanga, Mgambo ikashinda 1-0 na ilikuwa februari 9 mwaka 2014.
Leo hii timu hizi zinakutana kwa mara ya 5 katika mchezo namba 62 wa ligi kuu Tanzania bara ambapo awali ulitakiwa kucheza januari 4 mwaka 2015, lakini uliahirishwa kutokana na Simba kushiriki kombe la mapinduzi.
Simba hawajawahi kushinda Mkwakwani dhidi ya Mgambo, je leo wataweza kutafuna mfupa wa wanajeshi hao?
0 comments:
Post a Comment