Wednesday, March 18, 2015


Mgambo walimdhibiti vizuri Emmanuel Okwi leo Mkwakwani
Na Bertha Lumala, Tanga
Kikosi cha maafande wa Mgambo Shooting kimeifunza soka Simba SC na kuichapa mabao 2-0 Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa jioni hii.

Mabao ya Salim Azizi Gila dakika ya 45 na Malimi Busungu dakika 68 aliyefunga kwa penalti, yameifanya timu hiyo ya Kabuku, Handeni jijini hapa kulinda rekodi yake ya kutopoteza mechi dhidi ya Simba SC na Yanga SC kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu ipande daraja misimu miwili iliyopita.

Kikosi cha kocha mkuu Bakari Shime cha Mgambo Shooting Stars kilianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kupata kona ya dakika ya kwanza tu ya mchezo ambayo hata hivyo, haikuzaa matunda kutokana na ubora wa kipa Ivo Mapunda.
 
Katika kuthibitisha walikuwa wamedhamiria kushinda, Mgambo walimiliki mpira kwa muda mwingi kuzidi Simba SC huku wakipiga pasi fupi fupi na za uhakika.

Zilipotimia dakika 45 kipindi cha kwanza, refa Kudra Omar kutoka jijini hapa aliyekuwa mezani leo, aliongeza dakika tatu za kufidia muda uliopotea.

Katika dakika ya kwanza ya dakika hizo tatu za nyongeza, Mgambo walifanya shambulizi kali kupitia wingi ya kushoto mshambuliaji Malimi Busungu akapenyeza pasi kali iliyomkuta Gila nje kidogo mwa boksi akafumua shuti la nyuzi 90 na kuandika bao la kwanza kwa wenyeji lililodumu kipindi chote cha kwanza.

Nafasi nzuri zaidi za Simba SC kipindi cha kwanza zilikuwa nne, lakini hazikutendewa haki na washambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na Ibrahim Ajibu.

Okwi alijikuta akishika kichwa kwa dakika nzima kutokana na kupiga kicwa nje ya lango la Mgambo dakika ya 24 alipopenyezewa krosi murua na mchezaji pekee aliyepiga 'hat-trick' msimu huu, Ajibu. Kichwa cha Mganda huyo kilipita nje kidogo mwa nguzo ya lango la Kusini mwa Uwanja wa Mkwakwani.

Dakika mbili baada ya saa ya mchezo, Simba SC walifanya shambulizi kali la kushtukiza, lakini kipa Godson Mmasa aliruka juu na kipangua mpira kisha kuumia vibaya baada ya kugongana na Okwi.

Kipa huyo aligangwa uwanjani kwa dakika nne kisha akatolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kipa Said Lubawa ambaye pia alikuwa mwiba mkali kwa mashuti na mashambulizi ya wekundu hao wa Msimbazi.

Katika dakika ya 66 Mgambo walifanya shambulizi kali la kushtukiza Gila alipowatoka mabeki kisha kushikwa mguu ndani ya boksi na kipa Ivo ambaye refa Amon Paul kutoka Mara alimlima kadi nyekundu kutokana na kosa hilo.

Kipa kinda Peter Manyika Jr aliingizwa kudaka penalti hiyo akipishwa na kiungo mshambuliaji Said Khamis Ndemla.

Busungu aliyetoa pasi ya goli la kwanza, alipiga penalti hiyo na kufunga akimchambua kipa huyo likiwa ni goli la 7 kwake msimu huu.

Simba SC walijaribu kufanya mashambulizi kwa nguvu langoni mwa Mgambo, lakini maafande hao walikuwa wazuri zaidi pale walipounasa mpira.

Kama si ubora wa Manyika Jr, Simba SC ilikuwa hatari kufungwa zaidi ya mabao 6 kipindi cha pili na kuifanya timu hiyo ya Kabuku kulipa kisasi cha kufungwa mabao 6-0 jijini Dar es Salaam msimu uliopita kwani Busungu, Gila na Maganga walikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Simba SC baada ya timu yao kuwa pungufu kwa mchezaji mmoja.

Manyika Jr, mtoto wa kipa wa zamani Peter Manyika aliyefungua kituo cha kunoa makipa jijini Dar es Salaam, alidhihirisha ubora wake kwa kupangua mashuti mengi ya wakali hao wa mabao, baadhi yakizaa kona.

Benchi la ufundi la Simba SC lilitaka kumtoa Okwi ambaye dakika ya 13 kipindi cha kwanza aliumia na kulazimika kugangwa nje ya uwanja wa dakika 4 na kumuingiza Maguli, lakini Mganda huyo alionyesha ishara ya kwamba angeweza kuendelea na mechi.

Hata hivyo, Okwi ambaye amefunga katika mechi tatu zilizopita kabla ya mechi ya leo, ameshindwa kufanya la maana baada ya kupiga mashuti yaliyokwenda nje ama kudakwa na makipa wa Mgambo.
 
Licha ya kuongezwa dakika nane kufidia muda uliopotea, Simba SC haikufanikiwa kupata bao huku kocha mkuu, Mserbia Goran Kopunovic, akitumia mbio na kukacha kuongeza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo.

Kwa matokeo hayo, Simba SC imeendelea kubaki nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 29, tano nyuma ya wapinzani wao wa jadi Yanga SC, ambao leo wameipiga 2-1 Kagera Sugar FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vikosi vilikuwa;
Mgambo Shooting: Godson Mmasa/ Said Lubawa dk 62, Bashiru Chanacha/ Kheri Chacha dk 90, Salim Mlima, Ramadhani Malim, Salim Kipanga, Mohamed Samata, Malimi Busungu, Ally Nassoro, Novatus Lufunga, Fuluzulu Maganga na Salim Azizi Gila.

Simba SC: Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jomas Mkude, Abdi Banda, Said Khamis Ndemla/ Manyika Peter dk 66, Ibrahim Ajibu/ Elias Maguli dk 46, Emmanuel Okwi/ Simon Sserunkuma dk 80 na Ramadhani Singano.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video