Sunday, March 1, 2015

MKUTANO wa kawaida wa Wanachama wa Simba kwa mujibu wa katiba unafanyika asubuhi katika ukumbi wa Bwalo la Polisi, Osterbay, jijini Dar es salaam.
Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva amekaririwa akisema mkutano huu utakuwa na agenda moja muhimu ambayo ni kujadili mwenendo wa klabu katika mechi za ligi kuu.
Simba jana walishinda 5-0 dhidi ya Prisons katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Ibrahim Hajib 'Mido" alifunga magoli matatu 'Hat-trick' na mawili yakafungwa na Emmanuel Okwi na Ramadhan Singano 'Messi'.
Kabla ya mechi ya jana, Simba ilifungwa goli 1-0 na Stand United kule Shinyanga, na wiki moja kabla ya mechi hiyo ya CCM Kambarage, walishinda 2-0 dhidi ya Polisi Moro uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Ushindi wa jana umekuwa faraja kubwa kwa mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba. Timu yao haina mwenendo mzuri.
Simba imecheza mechi 16 na kujikusanyia pointi 23 katika nafasi ya nne ya msimamo.
Wameshinda mechi 5, sare 8 na kufungwa 3. Wamefunga magoli 20, wamefungwa magoli 12, wastani ni magoli 8.
Kukaa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi si jambo dogo, lakini inategemea wewe ni nani.
Unaposema Simba haifanyi vizuri lazima uwe na uwezo wa kutoa sababu. Kimpira bado matokeo yao ni mazuri. Kama Simba anafanya vibaya, Prisons, Mgambo JKT wanafanya nini?
Rais wa Simba, Evans Aveva

Kinachowafanya Simba waonekane ni uzoefu wao na heshima waliyokuwa nayo. Nyuma hawakuwa na matokeo kama haya, wamecheza ligi kwa muda mrefu, ni klabu ya pili kwa mafanikio katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa nyuma ya Yanga.
Simba, wanafainali wa kombe la CAF 1993, timu iliyocheza robo fainali ligi ya mabingwa Africa 2003 tena ikiwatoa Zamalek, mabingwa watetezi. Timu iliyotwaa ubingwa bila kupoteza mechi 2009/2010 ikiwa na Patrick Phiri, leo hii inakuwa timu ya kuungaunga, wengi ndipo wanaona haiwezekani.
Kiukweli Simba haijatulia tangu kipindi cha Aden Rage mpaka sasa Evans Aveva.
Timu ina mgogoro wa kiuongozi, Aveva ameshindwa kutengeneza umoja na kwa bahati mbaya sana yeye hakubali kama kuna tatizo kwenye uongozi wake.

Kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic

Haamini kama UKAWA wana athari, haamini kama kutokuwa na umoja nao ni tatizo. Ameshindwa kutegeu ukweli kwamba UkAWA wanaoshangilia majukwaani si hao tu, wapo wengi ambao wamejificha.
Leo hii unasikia makamu wa Rais, Geofrey Nyange Kaburu kazuiliwa kwenda kambini, mara anampangi kikosi kocha, anawagawa wachezaji. Haya yanazungumzwa na watu wa Simba na wasiokuwa wa Simba. Yote haya ni matokeo ya kukosa uweledi katika kazi ya kuongoza mpira.
Mbali na matatizo ya kiungozi ambaye yamekuwa na athari kubwa, Simba imeendelea kubadili makocha tangu 2012.
Wamepitia mikononi mwa Milovan Circovic, Patrick Liew, Abdallah Kibadeni, Zdravko Logarusic, Patrck Phiri na sasa Goran Kopunovic.
Makocha wote hao wana falsafa tofauti. Kuna wachezaji wamefanya kazi nao wote, unadhani kichwani wamehangaika vipi kuingia katika mifumo mipya mara kwa mara? 
Athari ya mabadiliko ya makocha imewakumba Simba. Kwa bahati Mbaya, Simba haijawa na wachezaji wa kazi kwa muda mrefu, waliowengi ni vijana wadogo wanaoendelea kujifunza mpira.
Wilium Lucian 'Gallas', Mohammed Hussein 'Tshabalala', Said Ndemla, Jonas Mkude n.k si wachezaji wa kutegemea wakupe ubingwa kwa haraka. Bado wanaendelea kujifunza.
Juzi nilikutana na kocha Kopunovic, alisema wazi kuwa timu yake ina vipaji vingi, lakini bado ni changa. Inahitaji muda, akasema haihitaji miaka 10, lakini anahitaji muda kukisuka kikosi chake.
Akaahidi kuwa msimu ujao, Simba itakuwa timu bora. Lakini wasiwasi wangu atafika huo msimu anaoutaka yeye?, Simba hawakubali kutoa muda hasusani wanapoona Yanga wanafanikiwa.
Leo hii wanachama wanakwenda kujadili mwenendo wa timu? kwa maani ipi? kiufundi waliowengi hawana elimu ya mpira. Zaidi wanasoma kwenye mitandao, magazeti, wanatazama kwenye TV na kusikiliza redio.
Kama wanakwenda kujadili mwenendo wa klabu katika Levo' ya uongozi na matatizo ya uongozi wao, hapo sawa, lakini swala la ufundi, waachie wataalamu wao wajadili.
Sidhani kama mkutano kama huo unaweza kuleta tija katika timu ya Goran. Wao wamalize migogoro ya kiuongozi, kocha aendelee na programu zake na wala wasihusishe mambo ya kiufundi.
Ni wakati muafaka wa kumaliza tofauti zilizopo Simba,Aveva akubali tu, asiwe mgumu wa kuamini anayotaka yeye na kushauriwa na maswahiba zake, awasikilize wanachama vizuri na waamue pamoja.
Kila la kheri Simba katika mkutano wenu!

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video